Noble Quran » Swahili » Sorah Al-'alaq ( The Clot )

Choose the reader


Swahili

Sorah Al-'alaq ( The Clot ) - Verses Number 19
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ( 1 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 1
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ( 2 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 2
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ( 3 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 3
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ( 4 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 4
Ambaye amefundisha kwa kalamu.
عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ( 5 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 5
Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ( 6 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 6
Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri
أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ( 7 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 7
Akijiona katajirika.
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ( 8 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 8
Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ( 9 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 9
Umemwona yule anaye mkataza
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ( 10 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 10
Mja anapo sali?
أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ( 11 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 11
Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ( 12 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 12
Au anaamrisha uchamngu?
أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ( 13 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 13
Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّهَ يَرَىٰ ( 14 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 14
Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ( 15 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 15
Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ( 16 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 16
Shungi la uwongo, lenye makosa!
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ( 17 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 17
Basi na awaite wenzake!
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ( 18 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 18
Nasi tutawaita Mazabania!
كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩ ( 19 ) Al-'alaq ( The Clot ) - Ayaa 19
Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!

Random Books

Choose language

Choose Sorah

Random Books

Choose tafseer

Participate

Bookmark and Share